Tiktok yapigwa marufuku

0
662

Tume ya Ulaya imepiga marufuku wafanyakazi wa Umoja wa Ulaya (EU) kutumia mtandao wa TikTok.

Hatua hiyo imefikiwa kufuatia Marekani na serikali za Magharibi kupiga marufuku matumizi ya mtandao huo unaomilikiwa na China kwa sababu za kiusalama, kufuatia uhusiano mbaya na Beijing.

Wafanyakazi wameamriwa kufuta programu tumizi hiyo kwenye vifaa vya kazi, lakini pia kuiondoa kwenye vifaa vyovyote binafsi vyenye programu zinazohusiana na kazi ama la, wafute programu zinazohusiana na kazi ikiwa wanataka kubakiza TikTok.

Tume imewapa wafanyakazi hadi Machi 15 mwaka huu kufanya hivyo ili kulinda taarifa na kuimarisha usalama wa mtandao.