Muhammad Mukhbar kuiongoza Iran siku 50

0
197

Makamu wa Rais wa Iran, Muhammad Mukhbar anajiandaa kuiongoza Iran ndani ya kipindi cha mpito, ambapo kwa sasa anasubiri kuthibitishwa na Kiongozi Mkuu wa Taifa hilo Ayatollah Ali Khamenei.

Mukhbar anachukua jukumu hilo kufuatia kifo cha Rais Ebrahim Raisi wa Iran kilichotokea baada ya helikopta iliyombeba kuanguka katika eneo la Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa katiba ya Iran, Rais mpya wa Taifa hilo ni lazima achaguliwe ndani ya kipindi cha siku 50 tangu kutokea kwa kifo cha Rais aliyekuwa madarakani.