Wachezaji wa kigeni Simba, Yanga na Singida hawajakidhi vigezo kushiriki Ngao ya Jamii

0
1001

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesema hadi sasa Azam FC ndio imewasilisha vibali vya wachezaji wa kigeni ambapo wataruhusiwa kucheza kwenye Ngao ya Jamii.

Wakati Azam ikiwa imesajili wachezaji 10, TFF imesema kuwa Singida Fountain Gate, Simba SC na Young Africans hazijasajili wachezaji wa kigeni.

Kutokana na hilo, TFF imesema hakuna mchezaji atakayeruhusiwa kucheza mashindano ya Ngao ya Jamii kama hatakuwa amekamilisha taratibu za kisheria.

Pazia la Ngao ya Jamii linafunguliwa leo kwa mchezo kati ya Young Africans dhidi ya Azam FC, huku Simba na Singida zikitarajiwa kushuka dimbani kesho.

Michezo yote itarushwa mbashara kupitia TBC Taifa na ukurasa wa YouTube wa TBCOnline.