Beno Kakolanya atoroka kambini

0
224

Golikipa namba moja katika kikosi Singida Fountain Gate FC Beno Kakolanya ametoroka kambini wakati timu yake ikijiandaa na mchezo wa Ligi Kuu dhidi Yanga SC utakaopigwa leo majira saa 10 jioni jijini Mwanza.

Taarifa iliyotolewa na uongozi wa klabu hiyo imesema kitendo hicho kinaleta maswali mengi hasa ukizingatia kuwa Beno ni mchezaji mzoefu na ni mmoja wa wachezaji wa kutumainiwa na timu ya Taifa.