Wadaiwa kumwacha Mchina ashinde

0
722

Uchunguzi unafanyika juu ya mashindano ya Beijing (Beijinga half marathon) kufuatia uwepo wa viashiria kuwa wakimbiaji watatu kutoka Afrika walipunguza mwendo kwa makusudi ili kuhakikisha mkimbiaji wa China, He Jie anakuwa mshindi.

Jie alimaliza mbio wa kwanza akitumia saa 1:03:44 akiwashinda wakimbiaji wa Kenya, Robert Keter na Willy Mnangat pamoja na Dejene Hailu kutoka Ethiopia.

Katika video iliyozua gumzo, wakimbiaji hao wanaonekana wakipunguza mwendo na kumwashiria Jie aongeze kasi apite mbele.

Tovuti ya Todayonline.com imemnukuu Mnangat akisema kuwa alimwacha Jie ashinde kwa sababu ni rafiki yake, kauli ambayo imedaiwa baadaye aliibadili na kusema kuwa alikuwa akimsaidie Jie (pacemaker).

Hata hivyo madai hayo yanaonekana si kweli kwani bango lake la ushiriki lilikuwa sawa na la Jie, na halikuwa limeandikwa ‘Pace’ kama ambavyo utaratibu hufanywa kwa wakimbiaji wanaomsaidia (pacemaker) mkimbiaji.