UTUNZAJI WA MAZINGIRA TIBA KWA AFYA YA AKILI

0
285

Kupitia Kampeni endelevu inayoendeshwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), ya upandaji wa miti nchi nzima. Leo tarehe 27 Julai 2023 zoezi la Upandaji miti limefanyika mkoani Dodoma katika na chuo Mipango ambapo Uongozi wa Chuo hicho umejitokeza kuunga mkono juhudi za utunzaji wa Mazingira.

Akizungumza na TBC, Makamu Mkuu wa Chuo cha Mipango Kitivo cha Taaluma, Prof. Provident Dimoso, amesema kuwa utunzaji wa mazingira kwa upandaji miti ni muhimu sana akieleza umuhimu wake kupitia tafiti ambazo zinaeleza kuwa utunzaji wa mazingira na upandaji wa miti unasaidia kutibu afya ya akili.

Vilevile ameongeza kuwa upandaji wa miti husaidia wanafunzi kuwa na akili bora timamu na imara na kusisitiza zaidi kuwa upandaji wa miti husaidia katika afya ya akili kwa mwanadamu kama tafiti zinavyoeleza kuwa miti hutoa hewa safi ambayo hupunguza kiwango cha msongo wa mawazo na kuboresha hali ya akili.

Kampeni ya Upandaji miti hufanyika kila tarehe 27 ya mwezi na huratibiwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).