TikTok yaruhusu ujumbe wa maandishi

0
327

Mtandao wa TikTok sasa kuwaruhusu watumiaji wake kuchapisha maudhui ya maandishi pekee bila ya video, hii ikiwa ni kwa mara ya kwanza kwa mtandao huo kufanya hivyo ikifuatiwa na ushindani wa kibiashara kutoka kwa mtandao pinzani ‘X’ uliokuwa ukifahamika awali kama twitter.

Mtandao huo umetangaza kuongeza wigo wa kupokea maoni na ubunifu kutoka kwa wataalam wengine juu ya namna ya kufanikisha zoezi hilo ikisisitiza kuwa upo tayari kupanua mipaka ya uundaji wa maudhui.

Sambamba na hilo matumizi ya ‘tags’ na ‘hashtags’ yamejumuishwa katika maboresho haya mapya ya mtandao wa TikTok.

Hapa awali mtandao wa TikTok ulikuwa ukiruhusu uundaji wa maudhui ya video na maandishi au video pekee bila ya maadhishi lakini sio ujumbe wa maandishi pekee.