Mloganzila yaingiza bilioni 8 kwa tiba urembo

0
184

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel amesema Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imezalisha shilingi Bilioni 8 kwa kufanya tiba urembo ambapo pia wameboresha maeneo mengi ya huduma ikiwemo ununuzi wa vifaa bora na vya kisasa na kuboresha chumba cha kuhifadhia maiti.

Amesema hayo wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI ambayo imeeleza kuridhishwa na hali ya utoaji huduma katika hospitali hiyo.

“Niipongeze Serikali kwa kuboresha huduma za afya nchini kwani hivi sasa asilimia 90 ya wagonjwa ambao walikuwa wanakwenda nje ya nchi kutibiwa wanatibiwa hapa nchini na tumeanza kupata wageni kutoka nje ya nchi kuja kupata huduma nchini,” ameeleza Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dkt. Faustine Ndugulile.

Aidha, ameitaka Serikali kupanua wigo wa utoaji huduma katika hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kwani hospitali hiyo bado ina eneo kubwa.