Mkandarasi Kiwanja cha Ndege Songea kukosa kazi

0
446

Naibu Waziri ametoa uamuzi huo kutokana na mkandarasi huyo kushindwa kukamilisha jengo hilo kwa wakati. Kihenzile ametembelea na kukagua maboresho makubwa yaliyofanywa katika kiwanja hicho.

“Serikali imewekeza shilingi bilioni 37 katika uwanja huu wa ndege, hivyo ni muhimu jengo la abiria likamilike kwa haraka. Nauelekeza uongozi wa TAA kuvunja mkataba na mkandarasi anayejenga jengo la abiria kwani ameshindwa kukamilisha ujenzi kwa wakati,” amesema.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Songea, Kapenjama Ndile amesema kuwa Kiwanja cha Ndege cha Songea ni muhimu kwa usafirishaji wa mizigo na abiria kutoka na kwenda nchi jirani za Msumbiji na Malawi. Faida nyingine amesema ni kutumika kusafirisha mazao mbalimbali hususani mbogamboga na matunda.

Jengo hilo la abiria lilitakiwa kukamilika mwezi wa sita mwaka jana lakini mpaka sasa lipo asilimia 30.