David Villa kustaafu soka hivi karibuni

0
1263

Mfungaji bora wa muda wote wa timu ya Taifa ya Hispania, – David Villa, ametangaza kustaafu soka mwishoni mwa mwaka huu ikiwa ni mwishoni mwa msimu wa Ligi Kuu ya Japan.

Nyota huyo wa zamani wa Barcelona amesema kuwa, kwa muda mrefu alikuwa akifikiria kustaafu soka kwani alitaka astaafu bila kulazimika kufanya hivyo, ambapo sasa anamalizia miaka yake 19 ya kulisakata soka la kiushindani.

Licha ya kushikilia rekodi ya ufungaji bora kwenye Taifa lake, pia nyota huyo ameshinda kombe la FIFA la Dunia la mwaka 2010 pamoja na ubingwa wa Mataifa ya Ulaya akiwa katika kikosi cha Hispania.

Kadhalika mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 37 ametwaa mataji mawili ya La Liga pamoja na taji la Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya akiwa na klabu ya Barcelona.

Villa amesema pamoja na kustaafu, ataendelea kujihusisha na mpira kwa njia nyingine na kuendelea kuchangia katika ulimwengu wa soka.