Mikoa hii wana ndugu wa asili Zanzibar

0
390

Rais Samia Suluhu Hassan akilihutubia Taifa usiku huu kupitia vyombo vya habari amesema undugu wa kihistoria ni chanzo cha Muungano kudumu kwa kuwa watu wa Tanganyika na Zanzibar kiasili ni wa jamii moja.

Akilihutubia Taifa kuelekea sherehe za Muungano hapo kesho Aprili 26, 2024 amesema watu wa Zanzibar na Tanganyika walitenganishwa kwa mipaka ya ukoloni pekee, lakini kwa asili walikuwa ni watu wa jamii moja na wengi wakifuatilia vinasaba vyao wanajikuta kuwa na chimbuko kutoka upande mmoja au mwingine wa Muungano.

Rais Samia ametolea mfano wenyeji wa mikoa ya Tanga, Pwani, Lindi, Mtwara, Morogoro, Mwanza, Shinyanga na Tabora na kusema kuwa wana ndugu zao wa asili kule Zanzibar.