Mihimili ya dola imefaidika kutokana na Muungano

0
120

Rais Samia Suluhu Hassan ametaja faida mbalimbali za Muungano ambazo ni pamoja na kuiwezesha Mihimili mitatu ya Dola kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa katiba kwa kushirikiana pande zote mbili za Muungano bila ya kuwepo na muingiliano.

Amesema kwa nyakati tofauti Muungano umetoa nafasi ya mageuzi kufanyika ndani ya nchi, ambapo baadhi ya mageuzi hayo ni kutambuliwa kwa haki za binadamu kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katiba ya Zanzibar.

Akilihutubia Taifa usiku huu kupitia vyombo vya habari kuelekea sherehe za miaka 60 ya Muungano Rais Samia ameongeza kuwa Muungano umesaidia kurejesha mfumo wa vyama vingi vya siasa mwaka 1992 pamoja na kuanzisha Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.