Toni Kroos kutundika daluga

0
192

Kiungo wa kati wa Real Madrid na Ujerumani, Toni Kroos ametangaza kutundika daruga baada ya michuano ya Uropa msimu huu.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 34 ametangaza uamuzi wake wa kustaafu soka kupitia ukurasa wake wa Instagram leo Jumanne.

Kroos ameamua kutoongeza mkataba wake na Real Madrid, ambao unamalizika mwishoni mwa msimu huu.

Kroos ameandika “Baada ya miaka 10, mwisho wa ukurasa huu unafikia tamati. Sitasahau kamwe wakati huo wa mafanikio! Ningependa hasa kumshukuru kila mtu ambaye alinikaribisha kwa moyo wangu wote hasa mashabiki wa Real Madrid”.

Kroos ambaye alitua Madrid miaka 10 iliyopita amekuwa na mchango mkubwa kwa klabu hiyo akiichezea michezo 463 na kutwaa mataji 22.

Kufuatia uamuzi huo, Rais wa Real Madrid amesema “Toni Kroos ni mmoja wa wachezaji nguli kwenye historia ya Real Madrid na kwamba Bernabeu kutaendelea kuwa nyumbani kwake”.