CCM yataka kukamilika barabara ya Kidatu- Ifakara

ZIARA MKOANI MOROGORO

0
82

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo ameuagiza Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kumsimamia mkandarasi anayejenga kwa kiwango cha lami barabara ya Kidatu – Ifakara yenye urefu wa kilomita 65.9 iliyopo mkoani Morogoro, ili aweze kukamilisha kazi hiyo kwa muda uliopangwa.

Akizungumza na wananchi mara baada ya kuwasili wilayani Kilombero akitokea wilayani Kilosa, Chongolo amesema haiwezekani ujenzi huo uchelewe wakati fedha za utekelezaji wake tayari zilikwishatengwa.

Chongolo ameonya kuwa wasimamizi watakaokaidi maelekezo hayo ya Chama Cha Mapinduzi watachukuliwa hatua.

Ujenzi wa barabara
ya Kidatu – Ifakara
ulioanza mwaka 2017 ulitakiwa kukamilika mwaka 2020 kwa gharama ya shilingi bilioni 105.035.