THPS yaipiga jeki sekta ya afya

0
165

Waziri wa afya Ummy Mwalimu ameyataka mashirika yote ya kiraia yanayofanya kazi na sekta ya afya, katika fedha wanazozipata watenge asilimia kumi kwa ajili ya kuajiri watumishi wa afya watakaotoa huduma kwenye vituo kwa ngazi ya msingi.

Waziri Ummy ametoa kauli hiyo jijini Tanga alipokuwa akipokea vitendea kazi vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 700 kwa ajili ya kusaidia sekta ya afya kwa ngazi ya msingi.

Vifaa hivyo vimetolewa na shirika la kiraia la
THPS ili kusaidia watu wenye maambukizi ya virusi vya Ukimwi pamoja na waraibu wa dawa za kulevya.