Watakiwa kuzingatia kanuni za afya kuepuka magonjwa

0
157

Ulaji usiozingatia misingi ya afya na mtindo wa maisha unatajwa kuchangia ongezeko la magonjwa yasiyo ya kuambuzika ambayo yanachangia ongezeko la wagonjwa wa figo.

Hayo yameelezwa na Dkt. Adam Gembe ambaye ni mkuu wa kitengo cha magonjwa ya ndani katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Pwani, Tumbi alipokuwa akizungumza katika kipindi cha Mirindimo ya TBC Taifa kutoka hospitalini hapo.

Aidha, amesema kwa sasa hospitali hiyo inahudumia wagonjwa takribani 12 kwa siku ambao wanapatiwa huduma ya kuchuja damu (dialysis).

Dkt. Gembe ametoa wito kwa watu kuzingatia kanuni za afya pamoja na matumizi sahihi ya dawa ili kuepuka magonjwa yasiyo ya kuambukiza ikiwa ni pamoja na shinikizo la damu, kisukari na saratani.