Tanzania kuendelea kushirikiana na AMCHAMTZ

0
139

Serikali imeahidi kuendelea kushirikiana na Chemba ya Wafanyabiashara wa Marekani na Tanzania (AMCHAMTZ) na Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) ili kufanikisha malengo ya AMCHAMTZ.

Kauli hiyo imetolewa mkoani Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara kutoka wizara ya Viwanda na Biashara Sempeho Manongi wakati wa uzinduzi wa Mpango Mkakati wa AMCHAMTZ wa mwaka 2024.

Manongi amesema mpango mkakati huo unaolenga kuimarisha biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Marekani ni hatua muhimu katika utekelezaji wa makubaliano ya U.S.-Tanzania Commercial Dialogue yaliyofikiwa na Mawaziri wa biashara wa nchi hizo mbili.