Watanzania waitwa kwa Mkapa

0
215

Serikali, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na wadau wengine leo wamehamasisha watanzania kuiunga mkono Taifa Stars katika michezo yake ijayo dhidi ya DRC na Madagascar na pia kuwaunga mkono Timu ya Taifa ya walemavu ya soka ambao ni wenyeji wa mashindano ya Afrika hapa nchini yatakayoanza mwishoni mwa mwezi huu.

Hayo yameelezwa Dar es Salaam leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi wakati wa mkutano na wanahabari Dar es Salaam kuhusu maandalizi ya Timu hiyo.

Kuhusu kwenda Madagascar Serikali na Kamati ya Kuhamasisha Taifa Stars, Dr. Abbasi amesema watakodi ndege aina ya AirBus.

Kuhusu Mashindano ya Walemavu Serikali iko nao katika maandalizi na itatoa zaidi ya shilingi milioni 135 kugharamia Timu, na nchi 16 zinazokuja kwa malazi, chakula na usafiri wa ndani.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidao amesema kambini kuna utulivu mkubwa na hakuna tatizo lolote na pia ameishukuru Serikali kwa kuhakikisha Timu inajiandaa vyakutosha.