Kocha wa Yanga afungiwa

0
731

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limemfungia kocha wa Yanga, Mohamed Nabi mechi tatu  za timu hiyo na kitozwa faini ya shilingi 500,000 kwa kosa la kinidhamu.

Kamati ya Mashindano ya TFF imechukua hatua hiyo baada ya kocha huyo kutiwa hatiani kwa kosa la kuwashambulia kwa lugha ya matusi waamuzi wa mchezo kati ya Yanga na Geita Gold FC, kitendo kilichopelekea kupewa kadi nyekundu.

Aidha, mchezaji wa Geita Gold, Kelvin Yondani amefungiwa michezo mitatu na  faini ya shilingi milioni 1 kwa kosa la kumkanyaga kwa makusudi mchezaji wa Yanga, Fiston Mayele, bila ya kuwa na mpira.

Pia, Yanga imepewa onyo kufuatia kitendo kisicho cha kimichezo cha washabiki wake kuwarushia chupa za maji wachezaji na bechi la ufundi la Geita Gold wakati wa wakiingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo wakati wa mapumziko katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC)