Mwenge wabisha hodi Tanga

0
285

Mwenge wa Uhuru umeanza mbio zake mkoani Tanga ukitokea mkoani Kilimanjaro, ambapo unatarajiwa kukimbizwa kwenye wilaya nane na halmashauri 11 za mkoa huo.

Mwenge huo umekabidhiwa kwa mkuu wa Mkoa wa Tanga, Dkt. Batilda Burian na Nurdin Babu ambaye ni mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Ukiwa mkoani Tanga, Mwenge wa Uhuru utazindua, kukagua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi 87 ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 40.

Kauli mbiu ya mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka huu ni Tunza mazingira na shiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa ujenzi wa Taifa endelevu.