Miaka 71 ya Wakunga, wawakumbuka wagonjwa

0
126

Watumishi wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania leo Machi 19, 2024 wameadhimisha miaka 71 tangu kuazishwa kwa baraza hilo kwa kukabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi Milioni tano katika Kituo cha Afya Makole kilichopo jijini Dodoma.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo
Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania Agnes Mtawa amesema, baadhi ya mafanikio yaliyofikiwa na baraza hilo tangu kuanzishwa kwake mwaka 1953 ni kuongezeka kwa idadi ya wauguzi na wakunga hadi kufikia 52,188, ujenzi wa mfumo wa kielektroniki wa kuhifadhi orodha na taarifa za wanataaluma, ujenzi wa kituo cha mafunzo wilayani Kibaha mkoani Pwani na mradi unaoendelea wa ujenzi wa ofisi kuu jijini Dodoma.