Kamati yatoa angalizo gharama za umeme

0
669

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imekagua utekelezaji wa miradi ya usambazaji umeme vijijini inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini ( REA) mkoani Pwani.

Akizungumza mara baada ya ukaguzi huo Mwenyekiti wa kamati hiyo Dkt. David Mathayo ameishauri Serikali kuangalia gharama za uunganishaji umeme kwa wananchi wanaoishi katika maeneo yanayotambulika kama Vijiji Miji ili kuwawezesha wananchi wengi zaidi kuunganisha umeme kwenye maeneo yao.

Pia ameshauri kuwe na usawa wa gharama za uunganishaji umeme kati ya wananchi wa vijijini na Vijiji Miji kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo zile za kiuchumi.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga amewashauri wakazi wa vijijini kutumia umeme kwa shughuli za maendeleo na kuchangamkia uunganishaji umeme kwenye maeneo yao pindi Serikali inapofikisha miundombinu ya umeme.