Yanga yavunja mkataba na Nkoma

0
424

Yanga SC imefikia makubaliano ya kuvunja mkataba na Kocha Mkuu wa Yanga Princess, Sebastian Nkoma.

Taarifa ya mtendaji mkuu wa klabu hiyo imeeleza kuwa uamuzi huo umefikiwa baada ya makubaliano ya pande zote mbili.

Kwa sasa benchi la ufundi litakuwa chini ya Koche Fredy Mbuna hadi mwisho wa msimu.

Kabla ya kujiunga Yanga, Nkoma alikuwa Kocha Mkuu wa Simba Queens kuanzia Novemba 2021 hadi Septemba 2022.