Shabiki afariki kutokana na vurugu Uwanja wa Mkapa

0
572

Mtu mmoja amefariki dunia na wengine 30 wamepata majereha sehemu mbalimbali za miili yao kutokana na vurugu zilizotokea katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Kuelekea mchezo wa kwanza wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Yanga SC na USM Alger ya Algeria, mashabiki walisababisha vurugu zilizopelekea kuvunjwa kwa geti la uwanja huo.

Akitoa taarifa kuhusu tukio hilo Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema “Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke imepokea majeruhi 30 ambapo 1 amefariki (Mwanaume mwenye umri wa takribani miaka 40.).

Ameongeza kuwa majeruhi wengi wanaendelea vizuri na kwamba wana majereha madogo madogo na wanaendelea na vipimo.

Aidha, Waziri wa Afya amesema timu kutoka Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ipo uwanjani, inafuatilia kwa karibu kuangalia kama kuna majeruhi wengine na timu ya wataalam wa Huduma za Dharura ya Hospitali ya Taifa Muhimbili  imeshawasiliana na Hospitali ya Rufaa Ya Mkoa Temeke na wapo tayari kupokea na kuwahudumia majeruhi ambao watahitaji matibabu zaidi.