Robo fainali ni kawaida kwa Simba

0
232

Afisa Habari wa Simba SC, Ahmed Ally amesema kuwa kufuzu hatua ya robo fainali kwa timu hiyo ni jambo la kawaida, na sio sherehe kama zinavyofanya timu nyingine

Amesema Simba imejipanga kushinda mechi yao dhidi ya Jwaneng Galaxy kwani kwa kufanya hivyo wataweka rekodi tatu ambazo ni kuingia robo fainali, kulipa kisasi na kuingia kwenye historia kuingia robo fainali mara nne mfululizo.

“Tangu tumeanza kampeni ya kimataifa hatujawahi kuishia hatua ya makundi, hatujawahi kufungwa mechi ya mwisho ya maamuzi ya kwenda robo fainali. Simba Sports Club inapofika hatua kama hii anakuwa mnyama mwingine wa ajabu,” amesema Ahmed Ally.

Simba inahitaji ushindi kufuzu hatua hiyo.