Waziri Jafo apanda mti TBC Arusha

0
122

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Selemani Jafo leo Aprili 27, 2024 amepanda miti ya matunda katika ofisi za redio jamii za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) mkoani Arusha akiunga mkono kampeni ya upandaji miti.

Waziri Jafo amepanda mti wa mwembe na kufanya jumla ya miti ya matunda katika ofisi hiyo kufikia 25 ikiwemo michungwa, mipera, miparachichi na mizambarau.

Pia Waziri Jafo amekagua maendeleo ya miti ya Kampeni ya #27yaKijani iliyopandwa katika eneo la TBC Arusha

Mpaka sasa kupitia kampeni ya #27yaKijani, Kanda ya Kaskazini imepanda jumla ya miti 3,000.

TanzaniaKijani #27yaKijani #TBCDigital #TBCArusha #Arusha #tanzania