Rais Samia afanya uteuzi

0
232

Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi wawili ambapo kwanza amemteua Stephen Wassira kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA).

Wassira ameteuliwa kwa kipindi cha pili cha miaka minne baada ya kipindi cha kwanza kumalizika.

Pili, amemteua Dkt. Fidelice Simbagungile Mafumiko, kuwa Mkemia Mkuu wa Serikali.

Simbagungile naye ameteuliwa kwa kipindi kingine cha miaka mitano kitakachoanza Aprili 3, 2023.