Dkt. Mwinyi aapisha mawaziri wapya

0
275

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.
Hussein Ali Mwinyi ameliagiza baraza la mawaziri kufanya kazi
kwa weledi ikiwemo kupambana na rushwa na ubadhirifu wa mali za
umma kwa maslahi mapana ya Taifa.

Dkt. Mwinyi ametoa maagizo hayo mara baada ya kuwaapisha
mawaziri wa awamu ya nane na kuongeza kuwa wahakikishe
wanatengezeza mpango kazi utakaoendana na ilani ya chama ikiwemo
utakelezaji wa ahadi unaoendana na dira ya maendeleo.

Zaidi, Dkt. Mwinyi amewataka mawaziri hao kuhakikisha wanazijua wizara zao na taasisi zilizoko chini ya wizara husika haraka iwezekanavyo.