Wanajeshi 50,000 wa Urusi wathibitika kuuawa

0
450

BBC Urusi, chombo huru cha Habari cha Mediazona na watu waliojitolea wamekuwa wakihesabu idadi ya wanajeshi wa Urusi waliouawa vitani tangu Februari 2022.

Makaburi mapya pia yamesaidia kutoa majina ya askari wengi. Timu zetu pia zilipitia ripoti huru, ripoti rasmi, magazeti na mitandao ya kijamii.

Zaidi ya wanajeshi 27,300 wa Urusi walikufa katika mwaka wa pili wa mapigano – kulingana na matokeo ya uchunguzi wetu.

Idadi jumla ya vifo ni zaidi ya askari 50,000. Kwa lugha nyingine ni mara nane zaidi ya idadi rasmi ya vifo iliyotangazwa na serikali ya Urusi kwa umma mwezi Septemba 2022

Lakini idadi halisi ya vifo inaweza kuwa kubwa zaidi. Uchambuzi wetu haujumuishi vifo vya wanamgambo huko Donetsk inayokaliwa na Urusi na Luhansk – mashariki mwa Ukraine. Wakijumuishwa, idadi ya vifo kwa upande wa Urusi itakuwa kubwa zaidi.

Ukraine nayo haitoi mara kwa mara idadi ya vifo katika uwanja wa vita. Mwezi Februari, Rais Volodymyr Zelensky alisema wanajeshi 31,000 wa Ukraine waliuawa – lakini makadirio ya idara ya ujasusi ya Marekani, yanaonyesha idadi ni kubwa zaidi ya hiyo.

Chanzo: BBC