Polisi mjini Bogota wapambana na waandamanaji

0
416

Polisi wa kutuliza ghasia mjini Bogota nchini Colombia wamepambana na waandamanaji waliokuwa wakishiriki katika maandamano ya kupinga sera za Rais wa nchi hiyo, ambazo wanasema hazina maslahi kwa wananchi.

Watu kadhaa wanashikiliwa na Polisi baada ya kuhusika katika ghasia zilizokuwa zikiambatana na maandamano hayo, ambayo yamesambaa katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo.

Tayari polisi wamewatia mbaroni watu kadhaa waliokuwa wakishiriki katika maandamano hayo kwa madai ya kuanzisha ghasia.