Makamu wa Rais wa zamani wa Marekani ashutumiwa kwa kutopinga ubaguzi

0
467

Makamu wa Rais wa zamani wa Marekani Joe Biden ameshutumiwa kutokuwa mstari wa mbele katika kupambana na vitendo vya ubaguzi wa rangi kwashirika wake wakati alipokuwa madarakani.


Biden amekabiliwa na shutuma hizo wakati wa mdahalo kwa wanachama ishirini wa chama cha Democrat wanaowania kuteuliwa na chama hicho kuwania urais wa marekani katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Novemba 2020.


Shutuma hizo dhidi ya Biden zimetolewa na Seneta Kamala Harris ambaye ni miongoni mwa wagombea hao, ambapo amesema Joe Biden alifanya kazi kwa karibu na maseneta wawili waliodaiwa kuwa ni wabaguzi wa rangi na kushindwa kukemea tabia ya maseneta hao hadharani.


Hata hivyo, Biden amesema amekuwa akitafririwa vibaya kwa kufanya kazi na maseneta hao ambapo amesema katika utawala uliopitwa wa Rais Barak Obama nchini Marekani, alikuwa kinara wa kupigania haki binaadam na kuleta usawa katika jamii, ikiwa ni pamoja na kupinga aina zote za ubaguzi nchini humo.