Maeneo hatari kwa watalii kutembelea duniani

0
462
Snake Island BR (China) - The Snake Island - ©UNESCO/Wang Ding

Duniani kuna baadhi ya maeneo ambayo yana sifa ambazo si za kuvutia.

Mamlaka za nchi husika zimepiga marufuku maeneo hayo kutembelewa, ama wameweka utaratibu maalum kwa watu kuzuru kwenye maeneo hayo.

Haya hapa ni maeneo hatari zaidi kuyatembelea

  1. Snake Island-Brazil- Ilha de Queimada Grande au Kisiwa cha nyoka

Kisiwa hiki kipo takribani maili 90 kutoka kwenye jiji la São Paulo nchini Brazil.

Inakadiriwa kuwa kuna nyoka elfu mbili wanaoishi katika kisiwa hicho chenye ukubwa wa mita za mraba laki nne na elfu 30, na hiyo ndio kusema kuna nyoka mmoja kila unapokaribia kumaliza mita za mraba kati ya moja hadi tano.

Martinique is a Caribbean island and is an overseas region of France.

Katika kisiwa hicho ndipo anakopatikana mmoja wa nyoka wenye sumu kali kabisa duniani, Golden Lancehead Viper (Bothrops insularis).

Wataalam wanasema sumu ya nyoka huyo ina nguvu karibu mara tano ya nyoka yoyote anayepatikana katika ardhi ya dunia kiasi cha kuweza kuyeyusha nyama ya mwili wa binadamu.

Jeshi la Wanamaji la Brazil limepiga marufuku mtu yeyote kutua ama kutia nanga katika kisiwa hicho cha nyoka isipokuwa tu kwa watafiti wa kisayansi wenye ruhusa maalum.

  1. Death Valley, eneo la kutisha

Bonde la kifo ni bonde la jangwa kwenye mpaka wa California na Nevada nchini Marekani na ni.eneo lenye joto kali.

Linajulikana kama moja ya maeneo yenye joto zaidi duniani.

Kuna majangwa machache tu katika Mashariki ya Kati na Afrika yanayokaribia joto kali wakati wa majira ya joto ambayo yanaweza kutoa ushindani kwa Bonde la Kifo.

A roadside sign warns visitors as they enter Death Valley National Park about extreme heat. Three hikers have died at the park this summer.

Joto la wastani pamoja na kiwango cha chini cha joto nyakati za usiku kilikuwa ni 108.1 ° F.

Kwa siku nne mfululizo viwango vya juu vya kila siku vilipiga joto la 127 ° F, likiwa ni joto la juu kabisa kuwahi kurekodiwa.

  1. Danakil Desert Ethiopia, eneo lenye milipuko ya volcano

Miongoni mwa maeneo yasiyokaliwa na watu duniani ni jangwa la Danakil katika Afrika Mashariki.

Kwa joto ambalo mara kwa mara huzidi 50 ° C (122 ° F), volkano na visima ambavyo vinatoa gesi yenye sumu, jangwa la Danakil sio eneo linaloweza kupatikana kwa urahisi kwa wapenda kusafiri.

Geological curiosity in the Ethiopian desert. (Wuthrich Didier / Shutterstock)

Afya ya mwili wa binadamu inaweza kubadilika ghafla akikaa katika eneo hilo kwa muda mfupi tu.

Tunaweza kusema kuwa eneo hilo la Danakil Desert ni miongoni mwa maeneo ya kushangaza zaidi duniani.

  1. North Sentinel Island

Ni kisiwa cha Sentinel Kaskazini ambacho kipo katika visiwa vya Andaman, kisiwa kinachotajwa kuwa moja ya maeneo hatari zaidi kwa watalii kutembelea.

Watu wa mahali hapo wamekuwa wakiishi kwa njia yao ya jadi na wamekataa njia zote zinazowezekana za kuungana na ulimwengu wa nje.

Watu wa kabila wanaoishi katika kisiwa hiki hawajazoea watu wa nje na ikiwa watalii wanakanyaga kisiwa chao, wanawaona kama tishio na kujiingiza katika vitendo vya vurugu.

  1. Madidi National Park, paradise mbugano yenye hatari kubwa

Hifadhi ya Taifa ya Madidi iko kando ya mto Amazon huko Bolivia na ina eneo la kilomita za mraba karibu elfu 19.

Hifadhi hiyo ambayo ni msitu mnene imejazwa na kila aina ya mimea na wanyama na aina zingine za mimea hatari na zisizofaa kuliwa.

Msitu huo mnene umejaa wanyama wanaokula wenzao, na ndio sababu watalii wanashauriwa kutotembelea hifadhi hiyo peke yao.

Msitu huo ni moja ya maeneo makubwa duniani yanayolindwa kwa kuwa una wanyama hatari, ndege na mimea hatari.

Je, unaishi katika maeneo yaliyoorodheshwa kuwa ni ya hatari zaidi kutembelea duniani,