Bashe aitwa Kilosa

0
232

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo ametoa muda wa wiki moja kwa waziri wa Kilimo Hussein Bashe kufika katika kijiiji cha Mvumi wilayani Kilosa, ili kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili wakulima wa kijiji hicho.

Chongolo ameyasema hayo wilayani Kilosa alipokuwa akizungumza na wakazi wa kijiji hicho ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku tisa mkoani Morogoro.

Ametaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na kutofanya kazi kwa skimu ya umwagiliaji ya Mvumi na kukosekana kwa maeneo ya kilimo licha ya Rais Samia Suluhu Hassan kufuta mashamba pori wilayani Kilosa.

Katibu Mkuu huyo wa CCM Taifa alikuwa akizungumza na wakazi wa kijiji hicho cha Mvumi akiwa njiani kuelekea mjini Kilosa na kusisitiza kuwa upo umuhimu wa wizara ya Kilimo kuajiri Mameneja watakaosimamia skimu za umwagiliaji nchini.