TASAC yazimulika bandari za Ziwa Tanganyika

0
3673

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) wameanza kutekeleza kwa vitendo agizo la Rais Samia Suluhu Hassan la kuufanya mkoa Kigoma kuwa kitovu cha biashara kwa mikoa ya magharibi na nchi za maziwa makuu kwa kuhakikisha wanasimamia imara vyombo vya usafirishaji majini kwenye ziwa Tanganyika ili kudhibiti usalama wa raia na mali zao.

Akizungumza na TBC, Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, Abdul Mkeyenge amesema wamejipanga kuhakikisha taratibu za kisheria za kimataifa na zile za Tanzania za  usalama wa usafirishaji majini ziwa Tanganyika kwa vyombo vinavyokwenda nchi za jirani Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na Zambia zinatekelezwa kikamilifu.

Mkeyenge ameongeza kuwa TASAC imejipanga kuongeza watendaji wake mkoani Kigoma ili kuhakikisha shughuli zinazohusiana na taasisi hiyo na wasafirishaji majini zinashughulikuwa kwa urahisi na kwa kipindi kifupi ili kusiwe na mkwamo kwenye utekelezaji wa shughuli za biashara na uchumi.