Mfumo mpya wa Google kuathiri maudhui yenye ubora duni

0
1043

Google mbioni kuzindua mfumo mpya utakaoathiri kuonekana kwa maudhui yenye kiwango cha chini cha ubora, mfumo ambao utaboresha upatikanaji wa taarifa katika kurasa zake.

Hapo awali waandaaji wa maudhui walikuwa wakitumia aina fulani ya maneno au njia ijulikanayo kama “SEO Freindly” yaliyowezesha maudhui yao kupatikana kwa wepesi juu katika ukurasa wa goolgle, pale mtumiaji atakapo kuwa anatafuta taarifa.

Afisa Uhusiano wa Umma na Ufuatiliaji wa Google, Danny Sullivan katika chapisho lake kwenye moja ya blog ameeleza kuwa maboresho hayo yataathiri zaidi maudhui yanayohusiana na utoaji wa elimu mitandaoni, maudhui ya sanaa na burudani, maudhui ya manunuzi mitandaoni na yale yanayohusisha masuala ya teknolojia.

Kwa upande mwingine, mfumo huo unaelezwa utakwenda mbali zaidi hadi kudhibiti kwa kuhakiki kurasa za kibiashara zinazotumia maoni ya kughushi kupitia mashirika au roboti ili kushawishi ununuzi wa bidhaa zao.