Instagram yatozwa faini Euro Milioni 405

0
1126

Mtandao maarufu wa kijamii wa Instagram umeshushiwa rungu la faini ya Euro milioni 405 na mamlaka yenye dhamana ya kutetea haki za watoto nchini Ireland.

Instagram imetozwa faini hiyo kufuatia malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa watu mbalimbali kuwa mtandao huo unakiuka haki za watoto kutokana na taarifa zao za muhimu kama namba za simu na anwani za barua pepe kuwekwa hadharani kutokana na akaunti zao kuwa za kibishara.

“Tulipitisha uamuzi wetu wa mwisho Ijumaa iliyopita na una faini ya Euro Milioni 405.” amesema kamishna wa ulinzi wa data wa Ireland

Kwa upande wake Afisa wa kampuni ya Meta alikiambia moja ya chombo cha habari kuwa uchunguzi uliofanyika ulikuwa umelenga mipangilio ya zamani ambayo kwa sasa imeshashushwa kwa zaidi ya mwaka mmoja uliopita na wameshatoa vipengele vingi vipya vitavyo saidia kuwaweka vijana salama na taarifa zao kuwa za faragha.

“Mtu yeyote aliye na umri wa chini ya miaka 18 akaunti yake inakuwa ya faragha moja kwamoja anapojiunga na Instagram, hivyo ni kwa watu anaowajua tu ndio wanaoweza kuona kile anachochapisha kupitia mtandao huo na watu wazima hawawezi kutuma ujumbe kwa vijana ambao hawawafuati “follow”. Alisema