Vifaa maalum kufungwa mipakani kuzuia dawa za kulevya

0
198

Serikali inatarajia kufunga vifaa maalum kwenye mipaka yote hapa nchini vitakavyoweza kufanya utambuzi wa upitishaji wa dawa za kulevya.

Kauli hiyo imetolewa jijini Tanga na Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya kuthibiti Dawa za kulevya nchini, Aretas Lyimo.

Amesema mara baada ya kufungwa kwa vifaa hivyo kutatolewa elimu ili kuwezesha taasisi zote 17 zinazofanya kazi kwenye mipaka kushirikiana katika kutokomeza uingizwaji wa dawa za kulevya.

Sambamba na hilo amesema mamlaka inajipanga kutoa elimu shirikishi kwenye jamii iishio jirani na mipaka kuhusu uthibiti wa dawa za kulevya kwenye maeneo yao.

Katika kipindi cha wiki moja Kamishna Jenerali Lyimo ametembelea mipaka iliyopo mikoa ya Laskazini mwa Tanzania ambayo ni Namanga, Holili, Tarakea na Horohoro.