Zanzibar yasitisha safari za baharini

0
261

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesitisha usafiri wa baharini na shughuli nyinginezo za baharini kuanzia leo Jumamosi, saa tatu asubuhi hadi pale taarifa nyingine zitakapotolewa na mamlaka husika.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Dkt. Khalid Salum Mohamed amesema serikali imefikia uamuzi huo ili kuchukua tahadhari ya dhidi ya Kimbunga Jobo.

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), kimbunga hicho kipo umbali wa kilomita 200 kutoka Kisiwa cha Mafia kikisafiri kwa kasi ya kilomita 18 kwa saa.

TMA imeeleza kuwa kasi hiyo imepungua kutoka ile iliyokuwa ikitarajiwa kutokana na kimbunga hicho kuingia katika mazingira yenye upepo kinzani.