Big up TBC, wengine igeni

0
96

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Selemani Jafo amelipongeza Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kwa kuendesha kampeni ya upandaji miti katika maeneo mbalimbali Tanzania.

“Kwanza nipende kuchukua fursa hii kwa leo hii kuwashukuru TBC kwa sababu mlianza tokea zoezi la Mti wa Mama na mimi nikiwa Waziri niliyepewa dhamana na mazingira nasema nawapa ‘Big up’ sana TBC kwa sabau mmeonesha mfano na nadhani wengine wanatakiwa waige mfano kama huu kila taasisi,” amesema Jafo

Jafo amayasema hayo baada ya kushiriki zoezi la kupanda miti ya matunda katika ofisi za redio jamii za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) mkoani Arusha.

TanzaniaKijani #27yaKijani #TBCDigital #TBCArusha #Arusha #tanzania