Maambukizi ya malaria Mtwara juu

0
139

Mkoa wa Mtwara umetajwa kuwa na maambukizi makubwa ya ugonjwa wa malaria kutoka asilimia 7.3 ambayo ni wastani wa kitaifa na kufikia asilimia 15.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ugawaji vyandarua katika kijiji cha Mpwapwa wilayani Newala kwa niaba ya Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas amesema hali hiyo inasababishwa na wananchi wengi wa mkoa huo kutotumia vyandarua na badala yake vyandarua huvitumia kwa shughuli za bustani na kufugia kuku.

Kanali Abbas amesema ili kuhakikisha maambukizi ya ugonjwa wa malaria yanapungua katika mkoa huo, serikali imekuja na kampeni ya kugawa vyandarua bure kwa wananchi wote.

Amesema Lindi na Mtwara ni miongoni mwa mikoa yenye maambukizi makubwa ya ugonjwa wa Malaria, hivyo jitihada zaidi zinahitajika kukakikisha kila mwananchi anatumia chandarua.