Likizo kwa wanaojifungua watoto njiti ni faraja

0
99

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Doris Mollel, Doris Mollel amesema tamko la serikali la kukubali ombi la kuongeza siku za likizo kwa wanaojifungua watoto njiti limetoa faraja kwa wanaojifungua kabla ya wakati na litasaidia kuongeza uangalizi wa watoto hao.

Uamuzi wa kuongeza likizo kwa wanaojifungua kabla ya wakati ulitangazwa na Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango, alipomwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika Sherehe za Kilele cha Mei Mosi Kitaifa zilizofanyika jijini Arusha.

Doris akiwa na wadau wengine wa masuala ya watoto njiti, amesema tangazo la serikali la kuruhusu likizo ya uzazi kuanza tu baada ya kumalizika kwa kipindi hicho cha uangalizi, kadiri madaktari watakavyothibitisha, linalinda ajira za wanaojifungua watoto njiti na kuwapa fursa ya kuwaaangalia watoto wao.