Dkt. Mpango kuhudhuria Stockholm +50

0
151

Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango amewasili Stockholm nchini Sweden ambapo anatarajiwa kuhudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Stockholm +50 utakaofanyika tarehe 2 hadi 3 Juni mwaka huu.

Dhumuni la mkutano huo ni kuchochea utekelezaji wa malengo endelevu ya Umoja wa Mataifa (Ajenda 2030) hususani katika upande wa mazingira na kujadili namna ya kurejesha uchumi endelevu katika kukabiliana na janga la UVIKO – 19.

Aidha mkutano huo ni maadhimisho ya miaka 50 tangu kufanyika mkutano wa kwanza wa mazingira wa Umoja wa Mataifa uliofanyika mjini Stockholm mwaka 1972.

Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Stockholm +50 unahudhuriwa na Wakuu wa nchi na serikali kutoka mataifa mbalimbali pamoja na wadau wa mazingira duniani.