Ajali Arusha yaua raia wa mataifa 7

0
430

Miongoni mwa watu waliofariki dunia katika ajali ya barabarani iliyotokea Februari 24, 2024 mkoani Arusha wana uraia wa Mataifa ya Marekani, Afrika Kusini, Nigeria, Togo, Bukinafaso, Madagasca na Kenya.

Katika ajali hiyo iliyotokea barabara ya Arusha Namanga, eneo la Ngaramtoni kibaoni, watu 25 walifarilki dunia na wengine zaidi wa 20 wamejeruhiwa.

Kufuatia ajali hiyo
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne Sagini amekagua eneo ilipotokea ajali hiyo na kutoa salamu za pole..

Pia ameliagiza Jeshi la Polisi nchini kuweka mikakati madhubuti ya ukaguzi wa magari yanayotoka nje ya nchi pamoja na yale yaliyopo ndani ya nchi pasipo kusubiri Wiki ya Nenda kwa Usalama ili kuepuka ajali zinazoweza kujitokeza kutokana na uzembe wa madereva ama ubovu wa magari