Tume ya Taifa ya Uchaguzi DRC (Ceni) yamtangaza Tshisekedi kuwa mshindi wa urais.

0
913

Tume ya Uchaguzi nchini Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo imesema kuwa Mgombea urais wa Upinzani Felix Tshisekedi ameshinda uchaguzi wa Rais nchini humo.

Matokeo ya uchaguzi ya awali kutoka katika majimbo mbalimbali yanaonyesha mgombea huyo wa upinzani amemshinda mgombea mwingine wa upinzani Martin Fayulu, pamoja na mgombea kutoka chama tawala Emmanuel Shadary.

Mkuu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Ceni) Corneille Nangaa, amesema mapema Alhamisi kwamba Tshisekedi alipata asilimia 38.57 ya kura zilizopigwa na anatangazwa mshindi wa urais mteule.

Tshisekedi alipata zaidi ya kura Milioni 7 huku Fayulu akipata kura takriban Milioni  6.4  na mgombea wa chama tawala Emmanuel Ramazani Shadary akipata takriban kura Milioni 4.4.

Tayari mgombea Fayulu ameyapinga matokeo hayo yaliyotangazwa na tume ya taifa ya uchaguzi.Kwa mujibu wa taarifa ya Idhaa ya kifaransa ya BBC  amesema kwamba matokeo hayo ni kashfa na haya uhalisia wa kweli.