Denmark kuendeleza ushirikiano na Tanzania

0
170

Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Denmark (DANIDA) limeadhimisha miaka 62 tangu kuanzishwa kwake hapa nchini huku Balozi wa Denmark nchini, Mette Norgaard Dissing-Spandet, akiahidi kuendeleza uhusino na ushiriano mzuri na wa muda mrefu baina ya nchi hizi mbili ulioanza tangu kipindi cha Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Balozi Mette amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuleta maendeleo ya kwa Watanzania na kwamba ameimarisha demokrasia na diplomasia baina ya mataifa duniani.

Akizungumza katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam leo Machi 22, 2024, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Asasi za Kiraia nchini (FCS), Francis Kiwanga amesema shirika hilo limekuwa mdau mkubwa wa pili hapa nchini kutoa ruzuku kwa FCS.

Katika ushirikiano wa miaka 14 na FCS, Kiwanga amesema msaada wa Danida umekuwa ukichangia kuziwezesha taasisi binafsi na asasi za maendeleo kukabiliana na umaskini hapa nchini.

Aidha, Kiwanga amepongeza juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan katika miaka yake mitatu madarakani, ambayo amesema ameimarisha misingi ya utawala bora, haki za binadamu, mifumo mizuri ya kusimamia rasilimali na uhuru wa watu kutoa maoni.