Wengine 463 wahama Hifadhi ya Ngorongoro

0
176

Wananchi 463 wamehama kwa hiari yao kutoka ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro kwenda Kijiji cha Msomera na maeneo mengine yaliyotengwa.

Hafla ya kuwaaga wananchi hao imefanyika leo Machi 19, 2024 na kuongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Kanali Wilson Sakulo.

Jumla ya kaya 77 zenye watu 463 na mifugo 1,408 ndizo zilizohama ndani ya hifadhi hiyo baada ya kujiandikisha na kuwa tayari kuhama kwa hiari.

Meneja mradi wa kuhamisha wananchi wanaohama kwa hiari kutoka Hifadhi ya Ngorongoro, Ofisa Uhifadhi Mkuu, Flora Assey amesema hadi kufikia wiki hii jumla ya kaya 1,195 zenye watu 7,195 na mifugo 33,064 zimeshahama ndani ya hifadhi hiyo.