Mtoto wa Gardner msibani Leaders

0
161

Mtoto wa Mtangazaji wa Clouds FM marehemu Gardner Habash, Kareen Habash akiwa katika viwanja vya Leaders Club mkoani Dar es Salaam ambapo ndugu, jamaa na marafiki wanatoa heshima za mwisho kwa mtangazaji huyo.

Gardner alifariki dunia Aprili 20, 2024 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo mkoani Dar es Salaam na atazikwa kesho Jumanne Aprili 23 huko Rombo mkoani Kilimanjaro.