Msimtenge Rais Samia

0
108

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara Abdulrahman Kinana amesema mtu yeyote asijaribu kumtenga Rais Samia Suluhu Hassan na watanzania kwa kutoa kauli za kiuchochezi ikiwemo ile ya kwamba Rais ni Mzanzibar.

Kinana amesema hakuna aliyekataa kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ni mzaliwa wa Zanzibar, lakini Katiba ya nchi inaruhusu Rais wa Tanzania kutoka Bara ama Zanzibar hivyo Rais aliyepo madarakani ni wa Kikatiba.

“Rais Samia amafanya vitu vingi Bara na Visiwani kwa maendeleo ya nchi kwa ujumla kama kujenga barabara, shule hata kuendeleza kujengwa kwa Makao Makuu Dodoma bila ya kujali ukanda, dini wala ukabila”. amesisitiza Kinana

Amesema hayo mkoani Dodoma wakati wa mkutano wake na wanachama wa CCM pamoja na wananchi mbalimbali.

Kinana amewataka watanzania kuwa na imani na Rais Samia na kuangalia zaidi mambo ya kimaendelo anayoyasimamia na kumuunga mkono kwani kila analolifanya ni kwa maslahi ya Taifa, huku akiwasisitiza wawapuuze wanaojenga chuki baina yao na Rais.