Kinana ahimiza waumini kuheshimu imani za wengine

0
158

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara Abdulrahman Kinana amesema, ni jukumu la Viongozi wa dini kuwaunganisha Watanzania,
kudumisha amani, umoja na mshikamano.

Kinana ametaka kuendelezwa kwa utamaduni wa kuheshimu imani ya kila mmoja kwa kutazama mambo mazuri na sio changamoto chache zinazojitokeza.

Ameyaaema hayo mkoani Dar es Salaam wakati wa mashindano ya kuhifadhi na kusoma Kuraani Tukufu, yaliyoandaliwa na Taasisi ya Aswhabu al-Kahfi Islamic Centre.

“Hivi sasa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweka mkazo kwenye maridhiano na tuna taasisi ya maridhiano na amani mbayo imeunganisha dini na madhehebu mbalimbali nchini, lengo ni kudumisha umoja, mshikamano na amani katika taifa letu”. Amesema Kinana na kuongeza kuwa
“Mimi ningependa kuwasihi viongozi wa dini, kila madhehebu, kila dini ni muhimu tushikamane na msitafute mapungufu ya kila mmoja, mtafute mema ya kila mmoja ili tuweze kushikamana”.