EAC yavutiwa na miradi mikubwa ya kimkakati nchini Tanzania

0
210

Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imeeleza kufurahishwa na miradi mikubwa na ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali ya Tanzania.

Hayo yameelezwa na Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia Mipango, Miundombinu, Fedha na Utawala Mhandisi Steven Mlote

Mhandisi Mlote ameyasema hayo wakati ujumbe kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki ulipotembelea mradi wa ujenzi wa bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere
na kuongeza kuwa mradi huo utakapokamilika utachochea ukuaji wa uchumi na biashara katika Jumuiya hiyo.
 
Ujenzi wa bwawa hilo la kufua umeme la Julius Nyerere unatarajiwa kukamilika mwezi Juni mwaka 2022 na kuzalisha Megawati 2115 za umeme. 
 
Ujumbe huo kutoka EAC umefurahishwa na taarifa kuwa mradi huo unafadhiliwa na fedha za Watanzania na umempongeza Rais Dkt John Magufuli kwa uthubutu wake wa kutekeleza mradi huo.
 
Awali ujumbe huo wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ulitembelea mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kwa lengo la kujionea maendeleo ya ujenzi na kueleza kufurahishwa na kazi kubwa inayofanywa na Serikali chini ya uongozi wa Rais Dkt John Magufuli.